Monday, October 31, 2011

Kazi Studioni


Kazi ikiendelea katika Studio ya Redio Pangani FM inayomilikiwa na shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA). Shirika hili ni miongoni mwa Washirika wakuu wa Ushirika wa Kusimamia Mazingira na Rasilimali za Pwani na Bahari ambao hurusha baadhi ya vipindi vyake vya mazingira katika redio hiyo 

Monday, October 24, 2011

Mambo ya Teknohama




Waandishi na watengenezaji vipindi vya redio na televisheni wakijifunza jinsi ya kuanzisha redio za intaneti kwa kutumia programu ya Podomatic katika Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo ya Kimataifa, IFM Dar Es Salaam. Ofisa Mawasiliano wa TCMP, Marko Gideon (hayupo pichani) alikuwa miongoni mwa washiriki katika mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika na Shirika la Maendeleo, Vyombo vya Habari na Mawasiliano (VIKES) la Finland Oktoba 24 - 28, 2011

Monday, October 17, 2011

Kilimo cha Miembe


Mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari hata kwa mazao ambayo hapo kabla yalistawi vizuri katika mazingira ya Pwani Yetu. Njia bora ya kukabiliana na hali hii ni kupanda mazao mbadala. Picha hapo juu inamuonyesha Dk. Shayo wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiangalia mwembe uliopandwa katika shamba linaloendeshwa na kamati ya mabadiliko ya tabia nchi ya kijiji cha Kitonga, Bagamoyo, kama njia ya kukabiliana na mabadiliko kwa kupanda mazao mbadala.