Uwezo Wetu

Tukiwa tunafanya kazi na watu, taasisi na washirika katika eneo husika,  sisi katika TCMP tunataka mazingira ya pwani kuruhusu wakazi wake kuwa wenye afya, wenye mafanikio, wenye nguvu na pwani yenye uwezo wa kiuzalishaji kwa ajili ya kukuza uchumi wa eneo hilo na watu wake. Hii ina maana kuwa na eneo ambalo watu wake wana uwezo wa kupata rasilimali bora ambazo wengi wao huzitegemea kwa chakula na kujiingizia kipato. Ina maana kuwa na eneo ambalo wakazi wake wanapata huduma za afya, elimu, na huduma za kifedha. Jambo muhimu zaidi hapa ni kuwa na eneo ambalo watu wake wote - ikiwa ni pamoja na wanaume kwa wanawake - wana sauti katika utoaji wa maamuzi ambayo yanatengeneza mustakabali wao wa baadaye. TCMP inajivunia kwa kuwa na mizizi katika maeneo ya jamii na kuwa na imani kuwa thamani halisi inatokana na kuwa na utambuzi juu ya utamaduni wao, mila na desturi, mahitaji na matakwa yao. Kwa hiyo tunafanya kazi zetu katika pwani na maji ya bahari ya Tanzania Bara na Zanzibar. Kuzidi kuongezeka kutambuliwa kwa kazi zetu, ikiwa ni pamoja na uzoefu wa washirika wetu, kumesababisha kuzidi kutambuliwa katika Afrika Mashariki na kimataifa.  TCMP  pamoja na mitandao yake inaweza kutoa aina mbalimbali za huduma za usimamizi wa kitaalam na kiufundi zinazohusiana na:
  • Maandalizi ya sera;
  • Mipango;
  • Ushauri na huduma za kitaalam;
  • Maandalizi ya miradi na utekelezaji wake;
  • Kuendeleza kipato;
  • Mikakati ya kuhifadhi mazingira, ikiwa ni pamoja na maeneo ya hifadhi ya bahari;
  • Kutatua migogoro kati ya watumiaji; kuingiza masuala mtambuka kisekta katika Mpango wa Pamoja wa Kusimamia Mazingira ya Pwani (ICM) kama zile:
  • VVU/UKIMWI,
  • maji na usafi wa mazingira, 
  • usawa wa jinsia, 

  • Mabadiliko ya tabia nchi, kujenga uwezo, kutoa mafunzo, ziara za mafunzo na huduma za ugani zinazofanywa na wataalam wa kusimamia mazingira ya pwani.