Tuesday, March 20, 2012

Jinsi Lulu Inavyoinua Kipato cha Wanawake wa Zanziabr






Nusu lulu ni ujasiriamali ambao umeinua kipato cha wanawake wengi wa Zanzibar. Shughuli hizi mbadala zimebuniwa kwa lengo la kuongeza kipato na wakati huo huo kuchochea hifadhi ya mazingira kwa kutunza miamba tengefu katika eneo zima la Ghuba ya Menai huko Unguja. Picha zinaonyesha jinsi vikundi vya wajasiriamali ambao wengi wao ni wanawake vilivyopata mafanikio katika kutengeneza lulu.

Wednesday, March 7, 2012

Mabadiliko ya Tabia Nchi ni Halisi

                                                                                         
"
Angalia jinsi mawimbi yalivyomomonyoa ukingo wa Bahari. Ukuta huu unaosemekana kujengwa miaka ya 80 katika eneo la Jambiani, huko Unguja, sasa umebaki kifusi                             

                              Hiki ni choo, ambacho kimechukukuliwa na mmomonyoko unaotokana na mawimbi makubwa ya bahari 

                                         
 Washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kusimamia Miradi inayofadhiliwa na Watu wa Marekani ulioandaliwa na Mradi wa TCMP-Pwani wakishuhudia athari za mabadiliko ya tabia nchi kandokando mwa Bahari ya Hindi katika eneo la Jambiani, huko Unguja

Majani haya katika mwambao wa Paje, Zanzibar, yanasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza athari za mawimbi ya bahari yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda wa pwani ikiwa ni pamoja na Zanzibar sasa ni halisi. Jamii zinaozishi karibu na bahari maeneo ya Bagamoyo, Pangani na Zanzibar zimeanza kushuhudia kuongezeka kwa nguvu ya mawimbi ya bahari na hivyo kuathiri makazi na shughuli zao za kiuchumi. Picha zinaonyesha mmomonyoko wa kingo za bahari unaosemekana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika eneo la Jambiani, Zanzibar. Pia zinaonyesha washiriki wa Mkutano wa Kamati ya Kusimamia Miradi inayofadhiliwa na Watu wa Marekani ulioandaliwa na TCMP-Pwani

Friday, March 2, 2012

Msitu wa Mikoko


Mikoko ni miongoni mwa miti adimu ambayo inahifadhiwa na serikali kisheria kutokana na umuhimu wake kwa bayoanuwai katika ukanda wa pwani. Umuhimu wake ni pamoja na kuwa mazalia mazuri ya samaki, kuzuia chembe chembe za mchanga zisifike baharini na kuyafunika matumbawe na pia katika kuhifadhi mazingira ya pwani kwa kuzuia mmomonyoko wa ukingo wa bahari na maingilio ya mito unaotokana na mawimbi makubwa ya bahari. Mikoko hutumika pia kama makazi, chakula na mazalia ya samaki wakubwa, kamba wadogo na chaza. Picha inaonyesha msitu wa mikoko katika kijiji cha Utondwe, wilayani Bagamoyo.