Friday, March 8, 2013

Kilimo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi


Moja ya kazi za kitengo cha mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani ni kuhamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahimili ukame, magonjwa na yanayokomaa haraka. Kazi hii inafanyika kwa kushirikiana na taasisi za utafiti wa kilimo nchini, wataalam wa kilimo wa wilaya, kata na katika ngazi ya kijiji. Mashamba ya ufuta bora yanaonekana katika kijiji cha Sange, Pangani.
 

Ofisa anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani, Bw Wilbard Mkama (kushoto) akitembelea mashamba ya majaribio ya kilimo bora cha ufuta katika kijiji cha Sange. Kulia ni bwana shamba wa kijiji hicho. 
 

 
 Migomba nayo ni zao ambalo limeonekana kuhimili ukame katika kijiji cha Mwembeni, Pangani.
 

Thursday, March 7, 2013

Mafunzo ya PHE

Mafunzo ya Idadi ya Watu, Afya na Mazingira (PHE) yaliyofanyika mjini Bagamoyo kuanzia tarehe 18 hadi 28 Februari yalikusanya wataalam wa mazingira kutoka nchi mbalimbali duniani. Mafunzo hayo yalikuwa ya vitendo zaidi. Juu kikundi cha kujadiliana kikiwa katika majdala mkali
 
Mafunzo yaliyokuwa ya vitendo zaidi yalitumia  dhana mbalimbali za kufundishia zilitumika
 
Michezo ya kuigiza pia ilitumika ili kufikisha ujumbe kwa washiriki katika mafunzo hayo