Kuhusu TCMP



Ushirika wa Hifadhi ya Mazingira ya Pwani na Bahari (TCMP) ulianzishwa rasmi mwaka 1997 kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania chini ya Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC), Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Marekani. Ushirika una lengo la kuhifadhi mazingira ya  pwani na bahari na wakati huo huo ukiinua kipato na kuboresha maisha ya wakazi wa pwani ya Mashariki mwa Tanzania.  Shabaha kuu ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uendelevu wa matumizi ya rasilimali za pwani na bahari kwa kuhifadhi mazingira na pia jitihada za makusudi zinachukuliwa kuhakikishia wananchi wanakuwa na kipato mbadala ili kuboresha maisha yao. Kipato kinapaswa kuwa endelevu kiasi cha kuwasaidia wananchi hao hata kama rasilimali za pwani zikiwa zimepungua kwa kiasi kikubwa.