Monday, November 12, 2012

Ujasiriamali Unaopunguza Matumizi ya Kuni




Rukia Seif wa kijiji cha Mkalamo akijishughulisha na kazi ya uokaji mikate katika jiko banifu. Picha ya chini ni Mkurugenzi wa Mradi wa Pwani, Baraka Kalangahe akiangalia jiko hilo katika ziara yake ya hivi karibuni ya kukagua shughuli zinazofanywa na wanavikundi wanaopata msaada kutoka Mradi wa Pwani katika wilaya ya Pangani. Jiko hilo banifu hutumia kuni chache, halitoi moshi mwingi na pia linamfanya Rukia kujishughulisha na shughuli ambazo ni rafiki kwa mazingira. 

Angalia Ujasiriamali na Uzazi wa Mpango



 
Mradi wa TCMP-Pwani unahamasisha matumizi ya dhana ya uzazi wa mpango na ujasiriamali katika kutunza mazingira. Pciha ya kwanza ikimuonyesha kijana akiwa amevaa fulana inayohamasisha uzazi wa mpango. Picha za chini zinaonyesha wanakijiji wa Sakura-Kwakiubuyu wilaya Pangani wakiwa katika biashara zao ndogondogo ambazo zinawafanya kuondokana na shughuli za uharibifu wa mazingira. Wajasiriamali hawa wamepata mikopo kutoka Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha Songambele. 

Tuesday, October 9, 2012

Kijijini Mwembeni, Pangani Jana

 Wanakijiji wa Mwembeni Baada ya Kukutana na wafanyakazi wa Mradi wa Pwani pamoja na waandishi wa habari na maofisa wa wilayani ya Pangani jana. Ziara hiyo ilikuwa ikifuatilia utekelezaji wa shughuli za mradi kijijini humo
 Wanakijiji wakielezea wageni wao jinsi kilimo cha mazao yaliyozoeleka kama mpunga, minazi na mahindi yalivyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuamua kuanza majaribio ya kilimo cha migomba


Mashina ya migomba inayostahimili ukame yakionekana yakianza kuchipua katika shamba la majaribio ya jinsi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika kijiji cha Mwembeni. Mashamba haya yameanzishwa na wananchi kwa kupata msaada wa ushauri na mbegu kutoka Mradi wa Pwani. Pia kupata msaada wa kitaalam kutoka halmashauri ya wilaya ya Pangani.

Takwimu za mashirika ya kimataifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu duniani wataanza kutegemea zaidi ndizi kama zao kuu la chakula kutokana na uwezekano wa mazao mengi ya chakula kushindwa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi.

Friday, September 28, 2012

Utunzaji wa Mikoko kwa Kufuga Nyuki


Baadhi ya Wanakamati ya Mazingira ya Kijiji cha Mlingotini wakipita katikati ya mikoko wakiwa katika mashua wakitoka kisiwa cha Mlingotini walikoweka mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki. Mizinga hii husaidia utunzaji wa misitu ya mikoko katika bahari.

Mizinga ya Nyuki ikiwa imeegeshwa kwenye miti ya mikoko katika Kisiwa cha Mlingotini, Bagamoyo
 

Bwana Shamba wa kijiji cha Pande akibadilishana mawazo na wafuatiliaji na waendeshaji tathmini ya mradi wa Pwani katika kisiwa cha Mlingotini ambako ufugaji wa nyuki unaendeshwa ili kuzalisha kipato na kutunza mazingira.

Misitu ya mikoko ina faida  nyingi kwa wanakijiji wa Mlingotini. Hapa mmoja wa wanakamati wa mazingira wa kijiji akiwa ameokota kuni zilizokauka kutoka katika msitu wa mikoko.

Friday, August 17, 2012

Kuwavua Tembo Kola


Kikosi cha angani kikijiandaa kupaa

Kikosi cha angani kikijiandaa kutua porini

                                        Kikosi cha ardhini kikielekea maeneo ya tukio

Kikosi cha ardhini kikikaribia eneo la tukio

Dk. Alfred Kikoti wa Kituo cha Utafiti wa Tembo Duniani akifanya kazi ya kuvua kola


Kazi ya kumvua tembo kola ikiendelea

Dk. Kikoti na mwenzake wakiangalia jeraha la risasi ambalo tembo aliyevuliwa kola alikuwa nalo. Hii inaonyesha kuendelea kwa vitendo vya ujangili dhidi ya nyara za taifa

Kazi imekamilika

Mradi wa Kufuatilia Mwenendo wa Tembo katika Mbuga ya Taifa ya Saadani na Pori la Hifadhi la Wambi Mbiki ulianza mwaka 2010 kwa kuwavisha tembo 17 kola ili kuweza kuwafuatilia kwa njia ya satelaiti. Baada ya kukusanya taarifa za kutosha, hivi majuzi kazi ya kuwavua kola hizo ilifanyika katika Pori la Hifadhi la Wami Mbiki kama picha zinavyoonyesha hapo juu. Mradi huo ni sehemu ya miradi iliyoko chini ya Mradi wa TCMP-Pwani unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID).
(Picha zote kwa hisani ya Dk. Alfred Kikoti wa Kituo cha Tembo Duniani)




























Wednesday, July 4, 2012

Angalia Pwani Yetu


Kilimo bora cha mpunga katika shamba la majaribio kwenye kijiji cha Kitonga, Bagamoyo ambalo linapata msaada kutoka Mradi wa TCMP-Pwani


Kilimo duni cha mpunga katika kijiji cha Sange, Pangani


Kilimo duni cha ufuta katika kijiji cha Sange, Pangani


Migomba yenye uwezo wa kustahimili ukame kwenye kijiji cha Mwembeni, Pangani. Kilimo cha aina hii ya migomba kinaweza kuwa njia nzuri ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo cha mazao ya chakula kwenye Pwani Yetu


Njia ya kuingia kwenye msitu wa asili wa Mziha, ambao unahifadhiliwa kwa imani za jadi kuheshimu "Mzimu wa Mziha" katika kijiji cha Mwembeni, Pangani. Maarifa ya jadi kama haya yanaweza kuhifadhi vizuri mazingira ya Pwani Yetu.




Muonekano bora katika maingilio ya Mto Msangazi katika kijiji cha Sange na Mto Pangani katika kijiji cha Msaraza wilayani Pangani. Maeneo haya yanahitaji kutunzwa ili kuhakikisha mazingira endelevu ya Pwani Yetu


Uhaba wa maji ni miongoni mwa changamoto nyingi zinazoikabili Pwani Yetu. Hali hiyo inazidi kujidhihirisha zaidi katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya tabia nchi yamepiga hodi kwenye vijiji vingi vya Pwani. Picha zikionyesha uhaba wa maji katika kijiji cha Mwembeni, wilayani Pangani.
Upandaji wa mimea aina ya Ipomea ni njia bora ya kuzuia mmomomyoko wa udongo ambao unasababishwa na kuongezeka kwa ukubwa na nguvu za mawimbi ya bahari katika Pwani Yetu. Hali hii inasemekana kuzidishwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Picha inaonyesha maandalizi  ya upandaji wa mimea hiyo katika ufukwe wa kijiji cha Sange.

Picha zote na Don Obadue wa Coastal Resources Center (CRC)

Friday, May 11, 2012

Mabadiliko ya Tabia Nchi ni Halisi




Buyuni ni moja ya vijiji vilivyoathirika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia nchi katika mwambao wa Bahari ya Hindi nchini Tanzania. Hali hiyo imefanya baadhi ya wanakijiji kuyahama makazi yao kutokana na maji ya bahari kuvamia makazi hayo. Picha zinaonyesha kijiji cha Buyuni kilichopo wilayani Pangani kama zilivyonaswa na mwandishi wa TCMP-Pwani leo asubuhi.

Tuesday, March 20, 2012

Jinsi Lulu Inavyoinua Kipato cha Wanawake wa Zanziabr






Nusu lulu ni ujasiriamali ambao umeinua kipato cha wanawake wengi wa Zanzibar. Shughuli hizi mbadala zimebuniwa kwa lengo la kuongeza kipato na wakati huo huo kuchochea hifadhi ya mazingira kwa kutunza miamba tengefu katika eneo zima la Ghuba ya Menai huko Unguja. Picha zinaonyesha jinsi vikundi vya wajasiriamali ambao wengi wao ni wanawake vilivyopata mafanikio katika kutengeneza lulu.

Wednesday, March 7, 2012

Mabadiliko ya Tabia Nchi ni Halisi

                                                                                         
"
Angalia jinsi mawimbi yalivyomomonyoa ukingo wa Bahari. Ukuta huu unaosemekana kujengwa miaka ya 80 katika eneo la Jambiani, huko Unguja, sasa umebaki kifusi                             

                              Hiki ni choo, ambacho kimechukukuliwa na mmomonyoko unaotokana na mawimbi makubwa ya bahari 

                                         
 Washiriki wa mkutano wa Kamati ya Kusimamia Miradi inayofadhiliwa na Watu wa Marekani ulioandaliwa na Mradi wa TCMP-Pwani wakishuhudia athari za mabadiliko ya tabia nchi kandokando mwa Bahari ya Hindi katika eneo la Jambiani, huko Unguja

Majani haya katika mwambao wa Paje, Zanzibar, yanasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza athari za mawimbi ya bahari yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda wa pwani ikiwa ni pamoja na Zanzibar sasa ni halisi. Jamii zinaozishi karibu na bahari maeneo ya Bagamoyo, Pangani na Zanzibar zimeanza kushuhudia kuongezeka kwa nguvu ya mawimbi ya bahari na hivyo kuathiri makazi na shughuli zao za kiuchumi. Picha zinaonyesha mmomonyoko wa kingo za bahari unaosemekana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika eneo la Jambiani, Zanzibar. Pia zinaonyesha washiriki wa Mkutano wa Kamati ya Kusimamia Miradi inayofadhiliwa na Watu wa Marekani ulioandaliwa na TCMP-Pwani