Baadhi ya Wanakamati ya Mazingira ya Kijiji cha Mlingotini wakipita katikati ya mikoko wakiwa katika mashua wakitoka kisiwa cha Mlingotini walikoweka mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki. Mizinga hii husaidia utunzaji wa misitu ya mikoko katika bahari.
Mizinga ya Nyuki ikiwa imeegeshwa kwenye miti ya mikoko katika Kisiwa cha Mlingotini, Bagamoyo
Bwana Shamba wa kijiji cha Pande akibadilishana mawazo na wafuatiliaji na waendeshaji tathmini ya mradi wa Pwani katika kisiwa cha Mlingotini ambako ufugaji wa nyuki unaendeshwa ili kuzalisha kipato na kutunza mazingira.
Misitu ya mikoko ina faida nyingi kwa wanakijiji wa Mlingotini. Hapa mmoja wa wanakamati wa mazingira wa kijiji akiwa ameokota kuni zilizokauka kutoka katika msitu wa mikoko.
No comments:
Post a Comment