Hakuna siri kuwa mafanikio ya kazi za TCMP yanatokana na mfumo wetu wa kuhakikisha kuwa matatizo na ufumbuzi wake vinaangaliwa kwa pamoja kama sehemu ya mfumo mzima badala ya kuangalia suala moja moja, iwe ni katika utungaji wa sera, kubuni kazi za mfano, kubainisha masuala ya msingi, kupanga mipango, kufanya tathmini, kutoa msaada wa kiufundi na hata kutatua migogoro. Mfumo huu unajikita katika kanuni ambazo zinatutaka kufanya kazi kwa njia ya:
- Kuunganisha sekta ;
- Kushirikisha wadau wote ; na
- Kuheshimu watu na tamaduni zao.
- Zinatumia maarifa na uzoefu wa wenyeji;
- Kutumia ushirikiano unaotambulika na usioegemea upande wowote katika kuwezesha mjadala na kutatua migogoro;
- Kuleta usawa wa rasilimali kwa ajili ya wote;
- Kuleta usawa katika jamii katika mambo yote tunayofanya ; na
- Kukuza uwezo katika ngazi ya jamii.
Copywright@TCMP 2011