Wafadhili Wetu


Ikiwa imenzishwa mwaka 1997, TCMP hadi sasa imekuwa ikifanya kazi kwa kiasi kikubwa kama mshirika wa Kituo cha Rasilimali za Pwani katika Chuo Kikuu cha Kisiwa cha  Rhode. Kiasi kikubwa cha ufadhili wake unatoka kwa wafadhili kama vile Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Benki ya Dunia na wafadhili wengine mmoja mmoja, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi. Hata hivyo, mwezi Agosti mwaka  2008, TCMP ilisajiliwa kama shirika lisilokuwa la kiserikali — na hivyo kuruhusiwa kupokea ufadhili na kutekeleza miradi kama chombo huru kisheria. Hadhi hii mpya ya shirika inalifanya kuwa na wigo mpana zaidi wa kupokea ufadhili kutoka kwa wafadhili ambao wangependa kusaidia kazi za  TCMP moja kwa moja ili kusaidia kazi zake nchini Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwa ajili ya mazingira bora ya pwani yetu.


 


Copyright@TCMP 2011