Tuesday, December 20, 2011

Samaki Hawa ni Urithi wa Pwani Yetu


Samaki aina ya Papa akiwa amevuliwa na wavuvi wa kijiji cha Ushongo wilayani Pagani, Tanga


Hawa nao wanachekelea kitoweo aina ya Pweza huko huko Ushongo, Pangani

Thursday, November 24, 2011

Ufugaji wa nyuki


Kuunga mkono au kuanzisha miradi mbadala ya kuwaingizia kipato wakazi wa maeneo ya mwambao wa pwani ni moja ya mfumo unaotumiwa na mradi wa TCMP Pwani ili kuifanya Pwani Yetu kuwa endelevu kwa kupunguza utegemezi wa kupindukia katika rasilimali za bahari.

Wednesday, November 9, 2011

Je wajua?


Mikoko ni moja ya rasilimali muhimu sana katika kuhifadhi mazingira ya pwani na bahari. Huzuia mmomonyoko unaosababishwa na mawimbi ya bahari na pia kutumika kama mazalia ya samaki. Angalia mikoko hii inavyopendeza.


Friday, November 4, 2011

Mkutano Umekwisha




Mkutano wa siku mbili ulihitimishwa na mazungumzo ya kuagana, kila mtu kubeba kilichokuwa cha kwake na picha ya pamoja tarehe 2/11/2011


Tuesday, November 1, 2011

Mkutano ukiendelea





Wafanyakazi wa TCMP na washirika wao wakiwa katika  kazi ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa Pwani kwa mwaka 2012 katika hoteli ya Livingstone, Bagamoyo. Mkutano wa siku mbili unamalizika kesho tarehe 2/11/2011. Kabla ya kuanza kwa mkutano asubuhi, kiongozi toka Baraza la Usimamizi wa Mazingira la Taifa (NEMC) Bw. Muheto anayeonekana katikati katika picha ya kwanza alitoa hotuba ya ufunguzi rasmi. Picha ya pili na ya tatu ni washiriki wakifuatilia ufunguzi huo. Picha ya nne ni mwakilishi wa mradi kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani (CRC) cha Chuo Kikuu cha Rhode Island Elin Torell akiweka kumbukumbu ya baadhi ya masuala yaliyojadiliwa.

Baada ya kazi kucheza



Wafanyakazi wa TCMP na washirika wao wakisakata rumba baada ya kazi ngumu ya siku nzima ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa Pwani kwa mwaka 2012 katika hoteli ya Livingstone, Bagamoyo. mkutano wa siku mbili unamalizika kesho tarehe 2/11/2011

Monday, October 31, 2011

Kazi Studioni


Kazi ikiendelea katika Studio ya Redio Pangani FM inayomilikiwa na shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA). Shirika hili ni miongoni mwa Washirika wakuu wa Ushirika wa Kusimamia Mazingira na Rasilimali za Pwani na Bahari ambao hurusha baadhi ya vipindi vyake vya mazingira katika redio hiyo 

Monday, October 24, 2011

Mambo ya Teknohama




Waandishi na watengenezaji vipindi vya redio na televisheni wakijifunza jinsi ya kuanzisha redio za intaneti kwa kutumia programu ya Podomatic katika Kituo cha Mafunzo ya Maendeleo ya Kimataifa, IFM Dar Es Salaam. Ofisa Mawasiliano wa TCMP, Marko Gideon (hayupo pichani) alikuwa miongoni mwa washiriki katika mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika na Shirika la Maendeleo, Vyombo vya Habari na Mawasiliano (VIKES) la Finland Oktoba 24 - 28, 2011

Monday, October 17, 2011

Kilimo cha Miembe


Mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari hata kwa mazao ambayo hapo kabla yalistawi vizuri katika mazingira ya Pwani Yetu. Njia bora ya kukabiliana na hali hii ni kupanda mazao mbadala. Picha hapo juu inamuonyesha Dk. Shayo wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiangalia mwembe uliopandwa katika shamba linaloendeshwa na kamati ya mabadiliko ya tabia nchi ya kijiji cha Kitonga, Bagamoyo, kama njia ya kukabiliana na mabadiliko kwa kupanda mazao mbadala. 

Friday, September 16, 2011

Angalia mazingira yanavyopendeza


Hebu fikiri mazingira ya Pwani Yetu yangekuwa mazuri kama bwawa hili katika kijiji cha Kitonga wilayani Bagamoyo.

Ukataji Miti




Biashara ya mkaa ni moja ya shughuli za binadamu zinazoharibu mazingira ya Pwani Yetu. Gari lililosheheni mkaa lilinaswa na mpiga picha wetu hivi karibuni katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta.