Friday, March 2, 2012

Msitu wa Mikoko


Mikoko ni miongoni mwa miti adimu ambayo inahifadhiwa na serikali kisheria kutokana na umuhimu wake kwa bayoanuwai katika ukanda wa pwani. Umuhimu wake ni pamoja na kuwa mazalia mazuri ya samaki, kuzuia chembe chembe za mchanga zisifike baharini na kuyafunika matumbawe na pia katika kuhifadhi mazingira ya pwani kwa kuzuia mmomonyoko wa ukingo wa bahari na maingilio ya mito unaotokana na mawimbi makubwa ya bahari. Mikoko hutumika pia kama makazi, chakula na mazalia ya samaki wakubwa, kamba wadogo na chaza. Picha inaonyesha msitu wa mikoko katika kijiji cha Utondwe, wilayani Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment