Moja ya kazi za kitengo cha mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani ni kuhamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahimili ukame, magonjwa na yanayokomaa haraka. Kazi hii inafanyika kwa kushirikiana na taasisi za utafiti wa kilimo nchini, wataalam wa kilimo wa wilaya, kata na katika ngazi ya kijiji. Mashamba ya ufuta bora yanaonekana katika kijiji cha Sange, Pangani.
Ofisa anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani, Bw Wilbard Mkama (kushoto) akitembelea mashamba ya majaribio ya kilimo bora cha ufuta katika kijiji cha Sange. Kulia ni bwana shamba wa kijiji hicho.
Migomba nayo ni zao ambalo limeonekana kuhimili ukame katika kijiji cha Mwembeni, Pangani.
No comments:
Post a Comment