Monday, May 6, 2013

SACCOS yasaidia kunyanyua kilimo Mkange

Shamba la mahindi na ufuta ambalo limelimwa kutokana na mkopo uliopatika kutoka SACCOS ya UWAMKE
Mwanachama wa SACCOS ya Mkange akiwa katika shamba lake la ekari nane ambalo amelima mahindi na ufuta kutokana na mkopo wa shilingi milioni mbili kutoka SACCOS hiyo.
Mratibu wa mradi wa kukuza uchumi wa TCMP Pwani Patrick Kajubili akiwa katika shamba la ufuta na mahindi la mwanachama wa SACCOS.

Mwenyekiti wa SACCOS ya Umoja wa Wanawake Mkange (UWAMKE), Mashavu Ali akiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Mkange katika shamba lake la ufuta kijijini hapo. Alianzisha shamba hilo kutokana na kukopa katika SACCOS hiyo.

Monday, April 8, 2013

Ziara ya Mshauri wa Kiufundi wa Masuala ya Idadi ya Watu, Afya na Mazingira wa USAID Matthew Erdman

Mjadala na vikundi vya SACCOS na Waelimishaji Rika Mkange
 
UZIKWASA ni mshirika mkuu wa TCMP Pwani wilayani Pangani
 
Kubadilishana uzoefu na taarifa na mkurugenzi wa UZIKWASA
 
Kugawa vifaa vya elimu na mawasiliano kwa Wasambazaji wa Vifaa na Huduma za PHE katika jamii (CBDs)
 
Picha ya pamoja na wadau wa Mkange
 
Picha ya pamoja na wadau wa Sakura
 
 
 
 
 
 

Friday, March 8, 2013

Kilimo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi


Moja ya kazi za kitengo cha mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani ni kuhamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahimili ukame, magonjwa na yanayokomaa haraka. Kazi hii inafanyika kwa kushirikiana na taasisi za utafiti wa kilimo nchini, wataalam wa kilimo wa wilaya, kata na katika ngazi ya kijiji. Mashamba ya ufuta bora yanaonekana katika kijiji cha Sange, Pangani.
 

Ofisa anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi katika mradi wa TCMP Pwani, Bw Wilbard Mkama (kushoto) akitembelea mashamba ya majaribio ya kilimo bora cha ufuta katika kijiji cha Sange. Kulia ni bwana shamba wa kijiji hicho. 
 

 
 Migomba nayo ni zao ambalo limeonekana kuhimili ukame katika kijiji cha Mwembeni, Pangani.
 

Thursday, March 7, 2013

Mafunzo ya PHE

Mafunzo ya Idadi ya Watu, Afya na Mazingira (PHE) yaliyofanyika mjini Bagamoyo kuanzia tarehe 18 hadi 28 Februari yalikusanya wataalam wa mazingira kutoka nchi mbalimbali duniani. Mafunzo hayo yalikuwa ya vitendo zaidi. Juu kikundi cha kujadiliana kikiwa katika majdala mkali
 
Mafunzo yaliyokuwa ya vitendo zaidi yalitumia  dhana mbalimbali za kufundishia zilitumika
 
Michezo ya kuigiza pia ilitumika ili kufikisha ujumbe kwa washiriki katika mafunzo hayo
 



Friday, February 15, 2013

Watoaji Huduma za Uzazi wa Mpango Katika Jamii

Watoaji Huduma za Uzazi wa Mpango (CBDs) katika jamii wana mchango mkubwa wa kupeleka huduma za afya na uzazi wa mpango karibu zaidi na jamii wanamoishi. Mmoja wa watoaji huduma hizo akiwa dukani kwake ambalo pia hutumika kama duka la kuuza kondomu katika kijiji cha Kwakibuyu/Sakura wilayani Pangani.